1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani imeyaaga mashindano ya kombe la dunia ya wanawake

10 Julai 2011

Timu ya taifa ya wanawake ya Japan imeifunga timu bingwa mtetezi Ujerumani 1-0 katika robo fainali za mashindano ya kombe la dunia ya wanawake mjini Wolfsburg

https://p.dw.com/p/11sNo
Kerstin Garefrekes wa timu ya Ujerumani apigwa na mshangao baada ya bao la JapanPicha: picture-alliance/dpa

Katika mashindano yanayoendelea ya Kombe la Dunia la wanawake, mabingwa watetezi Ujerumani, wametolewa kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Japan kunako dakika 120 ya mchezo huo.

Frauen-Fußball-WM Japan - Neuseeland Japan's Yuki Nagasato Tor
Wavu ulitikisika kwa kishindo cha MpiraPicha: dapd

Ushindi wa Japan mjini Wolfsburg umezima matumaini ya Ujerumani kujinyakulia mara ya tatu mtawalia, taji la mashindano haya.

Wakati huo huo, Japan imefuzu kwenye nusu fainali za mahsindano hayo na inatarajiwa kupambana na Sweden au Australia.

Frauen-Fußball-WM 2011 Viertelfinale Deutschland - Japan
Sherehe kwa JapanPicha: dapd

Mapema hapo jana, Ufaransa iliifunga timu ya Uingereza kupitia mikwaju ya penalti mjini Leverkusen na pia kufanikiwa kuingia kwenye nusu fainali hizo. Ufaransa sasa itakabiliana na Marekani au Brazil.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Zdf
Mhariri:Martin,Prema