1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Umoja wa Mataifa wakabidhi moja ya kambi za mwisho kwa Mali

Lilian Mtono
9 Desemba 2023

Vikosi vya walinda amani vilikabidhi moja ya kambi zake zilizosalia kwa mamlaka za Mali, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuondoka nchini humo kufuatia agizo la utawala wa kijeshi wa Mali.

https://p.dw.com/p/4Zxla
Umoja wa Mataifa waondoka Mali baada ya miaka kadhaa ya kupambana na makundi ya kigaidi
Umoja wa Mataifa waondoka Mali baada ya miaka kadhaa ya kupambana na makundi ya kigaidiPicha: Nicolas Remene/Le Pictorium/picture alliance

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Fatoumata Kaba ameliambia shirika la habari la AP kwamba, MINUSMA imekabidhi kambi ya Mopti iliyoko katikati mwa Mali, ambako ni moja ya maeneo yaliyoelemewa na uasi wa jihadi katika ukanda wa Sahel.

Kambi ya Mopti kwa kiasi kikubwa ilikaliwa na walinda amani kutoka Bangladesh na Togo na huko nyuma ilitumiwa na Misri, Pakistani na Senegal.

Siku ya Jumatatu MINUSMA itafanya tafrija ya kuifunga makao makuu yake katika mji mkuu Bamako, kuashiria mwisho wa ujumbe huo nchini Mali.