1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa waondoa wafanyikazi wake El Fasher

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm2

Umoja wa Mataifa umewaondoa baadhi ya wafanyikazi wake wa misaada kutoka mji wa El Fasher wa eneo la Darfur.Hatua hiyo inatokea kwasababu ya ongezeko la wapiganaji katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Radhia Achouri hatua hiyo ya muda imesababishwa na uhaba wa usalama kwasababu ya kuhofia vita kutokea kati ya wapiganaji wa Janjaweed na waasi.

Wafanyikazi mia moja kati ya mia tatu wameshaondolewa katika mji wa El Fasher jana usiku.Umoja wa Afrika umeonya kuwa makundi ya waasi huenda wakashambulia mji huo.

Wapiganaji wa Janjaweed na waasi wa SLM walipigana katika eneo la sokoni mwanzoni mwa juma na kusababisha vita vya waasi wawili.Kulingana na wataalam takriban watu laki mbili wamepoteza maisha yao katika vita kwenye eneo la Darfur na wengine milioni mbili u nusu kuachwa bila makazi tangu ghasia hizo kuanza mwaka 2003.