1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

UN: Tahadhari ya mapema ingelipunguza madhara Libya

Lilian Mtono
14 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema hii leo kwamba maelfu ya watu huenda wangenusurika na mafuriko nchini Libya ikiwa kungetolewa tahadhari ya mapema na kama mifumo ya usimamizi wa dharura ingekuwa inafanya kazi ipasavyo.

https://p.dw.com/p/4WLam
Mkuu wa shirika la Hali ya Hewa Umoja wa Mataifa Petteri Taalas
Mkuu wa shirika la Hali ya Hewa Umoja wa Mataifa Petteri TaalasPicha: FABRICE COFFRINI/AFP

Mkuu wa Shirika la masuala ya hali ya hewa la Umoja huo, WMO petteri Taalas amewaambia waandishi wa habari mjini geneva kwamba,  kama mifumo hiyo ingekuwa inafanya kazi sawasawa, wangeweza kuwahamisha wakazi na kuepusha vifo na majeruhi kama inavyoshuhudiwa sasa.

Taalas amesema kama kungekuwa na mifumo ya hali ya hewa inayofanya kazi kama kawaida, wangekuwa wametoa tahadhari na mamlaka za dharurazingeweza kuwahamisha wakazi.
  Soma pia:Juhudi za kuisaidia Libya zashika kasi

Saalas ametoa matamshi hayo baada ya upande wa Mashariki wa Libya kukumbwa na mafuriko ya kiwango cha Tsunami mwishoni mwa wiki iliyopita na kuua karibu watu 4,000, huku maelfu wakiwa hawajulikani walipo.