1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Walinda amani washambuliwa Mali

29 Novemba 2017

Mashambulizi 4 yamefanyika dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Kidal ulioko kaskazini mwa Mali

https://p.dw.com/p/2oS5n
Mali UN Mission MINUSMA
Picha: Getty Images/AFP/S. Rieussec

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mashambulizi manne yamefanyika dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja huo katika mkoa wa Kidal ulioko kaskazini mwa Mali, ingawa hakuna waliouawa au kujeruhiwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema kambi tatu za umoja huo katika maeneo ya Aquelhok, Tessalit na Kidal zilishambuliwa kwa roketi na makombora.

Amesema uchunguzi unaendelea kuwabaini waliohusika na mashambulizi hayo. Dujarric amesema wanajeshi waliokuwa katika doria kwenye mji wa Kidal walishambuliwa Jumanne asubuhi na kwamba mashambulizi hayo ni sawa na uhalifu wa kivita kulingana na sheria za kimataifa.

Kikosi hicho chenye wanajeshi 11,000 wa kulinda amani nchini Mali kimekuwa kikifanya kazi katika mazingira ya hatari zaidi duniani, ambapo mara kwa mara kinashambuliwa na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo hilo la kaskazini.