1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wadai kushinda uchaguzi Zimbabwe

Mohamed Dahman30 Machi 2008

Chama cha upizani cha MDC na Rais Robert Mugabe kila mmoja adai kuwa ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao ni wa rais,bunge na serikali za mitaa.

https://p.dw.com/p/DXNy
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai.Picha: picture-alliance/ dpa

Chama cha Upinzani nchini Zimbabwe cha MDC kimedai kushinda uchaguzi kwa kuzingatia kile inachosema kwamba matokeo ya awali ya uchaguzi huo mkuu uliofanyika hapo jana lakini Rais Robert Mugabe naye anadai kuwa amechaguliwa tena.

Chama cha MDC kinasema kiongozi wa chama hicho Morgan Tsvangirai alikuwa akitarajiwa kushinda katika mji mkuu wa Harare na ameweza kushinda kwenye ngome kuu za Mugabe katika majimbo ya Masvingo na Mashonaland.Katika mji mkuu wa pili kwa ukubwa wa Bulawayo chama cha MDC kimesema Tsvangirai amempita kidogo kwa kura Simba Makoni waziri wa zamani wa fedha ambaye pia anawania uchaguzi huo wa rais dhidi ya Mugabe.

Madai hayo hayakuweza kuyakinishwa na vyombo huru vya kujitegemea.

Mugabe kiongozi wa zamani wa wapiganaji wa kugombania uhuru wa nchi hiyo ambaye utawala wake wa miaka 28 umeiweka Zimbabwe kwenye ukingo wa kusambaratika kiuchumi ameyakataa madai kwamba alikuwa amepanga kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.

Mugabe amekaririwa akisema leo hii kwamba hakutakuwa na ulazima wa kufanyika kwa marudio ya uhaguzi kama katiba inavysomema wakati mgombea anaposhindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Mugabe mwenye umri wa miaka 84 amekariririwa na gazeti la Sunday Mail akisema wakiwa kama wagombea hawakuzoweya michunano ya masumbwi ambapo wapiganaji huanzia duru ya kwanza na kuendelea na kwamba huwa tu wanatwangana makonde na mmoja kumbwaga mwenzake nje ya ulingo.

Serikali imekionya chama cha MDC kwamba kisitangaze ushindi wake na kusema kwamba tangazo lolote lile litakalotolewa na Tsavangirai kwamba yeye ni mshindi aliestahiki kutakuwa sawa na kufanya mapinduzi.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi matokeo rasmi yataanza kutolewa leo hii.