1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatahadharisha juu ya mapigano Ossetia kusini

3 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/EpkF

Moscow:

Urusi imeonya kwamba mkoa wa Ossetia kusini uliojitenga na jamhuri ya Georgia mapema miaka ya 1990, unakaribia kuingia katika vmgogoro wa kijeshi mpana zaidi. hayo yanafuatia kukataa kwa Georgia madai kwamba majeshi yake yalihusika katika vifo vya watu sita katika mapigano ya Ijumaa na Jumamosi iliopita.

Georgia inamelaumu juu ya kile ilichokiita uchokozi wa waliojitenga, wakati jimbo hilo la Ossetia kusini likiilaumu Georgia kwa mashambulio ya risasi na kusema inawahamisha mamia ya watoto kuwapeleka Urusi. Urusi ina wanajeshi jimboni humo ambao inasema wanasimamia amani.

Georgia inayowania kujiunga na Shirika la kujihami la magharibi NATO, imeishutumu Urusi kuwa inataka kuitwaa mikoa ya Ossetia kusini na Abkhazia.