1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaondolewa katika mpango wa ndege chapa F-35

Sekione Kitojo
18 Julai 2019

Ikulu ya Marekani, imethibitisha kuwa Uturuki itaondolewa kutoka mpango wa ndege za kivita chapa F-35 baada ya kununua mfumo wa kuzuwia makombora kutoka Urusi ikikaidi onyo kutoka washirika wake wa mataifa ya magharibi. 

https://p.dw.com/p/3MFJE
Israel Kampfflugzeug Air Force F-35
Picha: Reuters/A. Cohen

Msemaji wa Ikulu ya Stephane Grisham amesema katika taarifa kuwa uamuzi wa  Uturuki kununua mfumo  wa  Urusi  wa  S-400  wa  kukinga  makombora  unafanya ushiriki wake  katika mafunzo ya  ndege  chapa F-35  kushindikana. 

Ndege  hizo zilizotengenezwa  nchini  Marekani chapa  F-35 , haziwezi  kufanyakazi  pamoja  na  jukwaa  la  ukusanya  taarifa  za kiintelijensia  la  Urusi  ambalo litatumika  kujifunza  juu  ya uwezo wake  wenye mbinu za kisasa  zaidi, amesema  Stephanie Grisham.

F-35 Kampfjet
Ndege za Marekani F-35Picha: picture-alliance/AP Photo/F. Hanson

Wizara ya mambo  ya  kigeni  ya  Uturuki  imeieleza  hatua  hiyo kuwa  si  ya  haki,  ikisema  katika  taarifa  kuwa , hatua  hii  ya upande  mmoja  haiendi pamoja  na moyo  wa ushirikiano  wa jumuiya  ya  NATO  na  wala  haiko  katika  misingi  ya  sababu halali.

Grisham  amesema  kuwa Marekani  imetoa maombi  kadhaa  ya mfumo  wake  wa  ulinzi dhidi  ya  makombora  wa  Patriot kwa Uturuki, lakini  Ankara  iliendelea  na  ununuzi wa  mfumo  wa  S-400, unaokwenda  kinyume  na  ahadi  za  ANTO kuepusha  kutumia mifumo  wa  Urusi.

"Hatua  hii  itakuwa  na  athari  kubwa  kwa  Uturuki  katika operesheni  zake  na  jumuiya  ya  NATO,"  amesema.  Grisham ameongeza  kuwa Marekani "bado  inadhamini  sana" uhusiano wake  wa  kimkakati  na  Uturuki  na  itaendelea  kushirikiana  nayo kwa  kiasi  kikubwa, kwa  kutafakari  juu  ya utata  uliopo kutokana na  kuwapo  na  mfumo  wa  S-400  nchini Uturuki.

Russisches Flugabwehrsystem S-400 für Türkei
Mfumo wa kukinga makombora wa Urusi wa S-400 ukipakuliwa nchini UturukiPicha: picture-alliance/dpa/Russian Defence Ministry

Mfumo wa S-400

Tangazo  hilo limekuja  siku  tano  baada  ya  Uturuki  kuanza kupokea  mfumo  wa  makombora  wa  Urusi , ikikaidi miaka  miwili ya onyo  kutoka  Marekani  na  mataifa  mengine  washirika  wa NATO kwamba  hatua  hiyo  inaweza  kuathiri  uhusiano  wao.

Hatua  ya  marekani  itayatenga makampuni  kadhaa  ya  Uturuki yanayotengeneza  baadhi ya sehemu  na  vipuri  vya  ndege  za kijeshi  chapa F-35, na  kuzuwia  mipango  ya  Uturuki  kununua ndege  hizo 100  za  kivita.

Siku  ya  Jumanne , rais Donald Trump  alikataa  kuishutumu  Uturuki kutokana  na  kununua  mfumo  huo wa S-400, akisema  kuwa  rais Recep Tayyip Erdogan amelazimika kuchukua  hatua  hiyo na mtangulizi  wake  katika  Ikulu  ya  Marekani  Barack Obama.

Hali hii itakuwa ni  upotevu  mkubwa  wa  mapato  kwa  kampuni  ya marekani  ya  Lockheed Martin  inayounda  ndege  hizo.

S-400 Luftabwehrsystem
Mfumo wa S-400 wa Urusi Picha: Getty Images/AFP

Uhusiano kati ya  Uturuki  na  Marekani umeathirika  kwa miaka kadhaa  sasa, kwa  sehemu  fulani  kutokana  na  mzozo  nchini Syria, pamoja  na ushirika  wa  marekani  na  wapiganaji  wa  Kikurdi nchini  Syria ambao Ankara  inawaona  kuwa  na  magaidi. Wizara ya  mambo  ya  kigeni ya  Uturuki imesema Marekani  inapaswa kuonesha  kwamba  inathamini  uhusiano  uliopo wa  kimkakati , kwa kupambana  dhidi ya  makundi  ya  kigaid.