1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vinu bado vimoto Japan

16 Machi 2011

Moto mwingine umezuka katika kinu nambari 4 cha Fukushima nchini Japan hii leo Jumatano.

https://p.dw.com/p/10Zgk
Kinu nambari 4 cha Fukushima Dai-ichi .Picha: AP

Wataalamu wa kampuni inayokisimamia kinu hicho, Tokyo Electric Power, wanasema vyuma vya mafuta katika eneo la kupoesha la kinu nambari 4 cha Fukushima kilichoathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea nchini Japan, huenda vikawa wazi kutokana na moto huo na vikatowa miale zaidi ya nyuklia hewani.

Japan Erdbeben 16.02.2011
Picha: AP

Hapo jana maafisa wa serikali nchini humo waliwaomba wakaazi waliopo umbali wa kilomita 30 kutoka kwenye kinu hicho, wahame au wajifungie ndani baada ya viwango vyenye athari vya miale hiyo ya nyuklia, kugunduliwa, kufuatia miripuko katika vinu nambari 1 na 4.

Janga lililopo Japan limesababisha kushuka kwa masoko ya hisa kote ulimwenguni, huku faharasha ya Nikkei ya Japan ikishuka kwa kiwango kikubwa tangu mwaka 2008 na DAX ya Frankfurt ikishuka kwa asilimia 3. Wakati huohuo hapo jana matetemeko mengine madogo ya ardhi yalidhihirika mashariki mwa nchi hiyo, siku nne baada ya eneo hilo kuathirika na tetemeko kubwa la ardhi lenye viwango vya magnitudi 9.0, na kusababisha kutokea tsunami.

Japan Pressekonferenz Atomkrise Fukushima Reaktor 16.03.2011
Wafanyakazi wa kampuni inayosimamia vinu vya nyuklia Japan, Tokyo Electric Power.Picha: AP

Idadi ya watu waliofariki inatarajiwa kuzidi watu 10,000, huku maafisa wa uokowaji wakiendelea kutafuta maiti.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Afpe,Ap,Dpa,Rtre