1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mkutano wa G20 India waafikia tamko la pamoja kuhusu Urusi

Tatu Karema
9 Septemba 2023

Viongozi wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi la G20 wanaokutana nchini India, wamekubaliana kutoa tamko la pamoja linaloepuka kuilaani Urusi katika vita vinavyoendelea Ukraine

https://p.dw.com/p/4W97f
Waziri mkuu wa India Narendra Modi (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan wakati wa mkutano wa G20 nchini India
Waziri mkuu wa India Narendra Modi (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan Picha: DHA

Makubaliano juu ya tamko hilo yamepatikana baada ya mvutano, wakati kundi hilo likiwa na mgawanyiko kuhusu vita nchini Ukraine ambapo awali nchi za Magharibi zilikuwa zikishinikiza kuilaani vikali Urusi huku mataifa mengine yakitaka lijikite katika masuala mapana ya kiuchumi.

Kumekuwa na ugumu katika kufikia makubaliano

Waratibu wamekuwa wakiripoti ugumu wa maelewano ya kutosha miongoni mwa mataifa hayo ya G20 ili kutoa tamko la la pamoja wakati wa mikutano ya kilele na kutaja masuala ya kisera yanayopaswa kushughulikiwa pamoja na mwelekeo wa shughuli za kongamano hilo.

Putin na Xi Jinping walitangaza kutohudhuria kongamano

Kuelekea Kongamano hilo, Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping walisema hawatahudhuria kongamano hilo, na kusababisha pigo kwa uhalali wa hafla hiyo ya kidiplomasia ya kila mwaka.