Vuta ni kuvute na Swala la Gesi nchini Tanzania

Bado swala la usafirishaji wa gesi inayopatikana katika eneo la Mtwara nchini Tanzania kwenda jijini Dar es Salaam linaendelea kuzua vuta ni kuvute kati ya serikali na wakaazi wa eneo hilo.

Wakaazi wa mkoa wa Mtwara hapo jana walilalamika kuwa ni lazima wafaidike na gesi iliyopatikana huko kabla ya kulinufaisha taifa zima.

Masuala ya Jamii | 03.01.2013

Hata hivyo waziri wa nishati na madini nchini Tanzania, Profesa Sospeter Muhungo, amesema kuwa haoni madai ya msingi kwa malalamiko hayo.

Amin Abubakar amezungumza naye na kwanza anaeleza zaidi juu ya suala hilo.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Josephat Charo.

Makala zaidi

Tufuatilie