1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya upinzani havitashiriki uchaguzi Sudan

3 Aprili 2010

Je, uchaguzi huo utaendelea kama ilivyopangwa?

https://p.dw.com/p/MmSK
Rais wa Sudan Omar Hassan al BashirPicha: DW/AP

Vyama vikuu vya upinzani nchini Sudan vimetishia kususia uchaguzi mkuu ujao wa vyama vingi nchini humo uliopangwa kufanyika baadaye mwezi huu kutokana na wasi wasi wake kuhusu hila katika uchaguzi na hali ya kutokuwepo usalama jimboni Darfur.

Hali hii inatishia kuharibu zoezi zima la uchaguzi nchini humo. Grace Kabogo alizungumza na Katibu Mkuu wa zamani wa uliokua Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU, Dr. Salim Ahmed Salim, ambaye pia aliwahi kusimamia mazungumzo ya amani ya Darfur na kwanza alitaka kupata mtazamo wake kufuatia hatua hiyo ya vyama vya upinzani.