1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi Syria wataka sasa kuwekwa zoni za kutoruka ndege

1 Juni 2013

Hali ya kurudishwa nyuma kwa waasi imesababisha waungaji wao mkono kutoa wito wa kuingilia kati zaidi kijeshi kwa Marekani ili kuweza kuwapa waasi karata yenye nguvu katika majadiliano kabla ya mazungumzo ya amani.

https://p.dw.com/p/18i9E
Louay al-Safi, spokesman for the Syrian National Coalition (L), speaks during a news conference in Istanbul May 26, 2013. Talks by Syria's opposition to choose a new leadership before an international peace conference stalled on Sunday over proposals to lessen Qatar's influence on the rebel forces, opposition sources said. REUTERS/Akin Celiktas (TURKEY - Tags: POLITICS)
Msemaji wa muungano wa kitaifa nchini Syria Louay al-SafiPicha: Reuters

Hususan baadhi ya waungaji mkono upinzani wanatoa wito kwa rais Barack Obama kuchukua hatua zaidi kupindukia ile ya kupeleka silaha tu kwa makundi maalum ya waasi yaliyochaguliwa, chaguo ambalo utawala huo unaripotiwa kuwa umo katika hali ya tafakari tangu ripoti kujitokeza mwezi uliopita kuwa jeshi la Syria limetumia silaha za kemikali dhidi ya waasi.

Kutokana na hali ya sasa ya udhaifu wa upinzani, wanadai kuwa , haina maana kwenda katika majadiliano mwezi huu mjini Geneva na wawakilishi wa serikali ya rais Bashar al-Assad , kama ilivyopendekezwa na Marekani na Urusi, bila kwanza kujaribu kubadilisha hali ya mambo katika vita.

epa03672845 German Foreign Minister Guido Westerwelle awaits the start of an EU Foreign Affairs Council at the EU Headquarters in Luxembourg, 22 April 2013. The European Union is to lift sanctions relating to oil exports and imports to opposition-controlled parts of Syria until 01 June 2013, according to a draft document to agreed by the bloc's foreign ministers on 22 April 2013. EPA/NICOLAS BOUVY
waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: picture-alliance/dpa

Zoni za kutoruka ndege

Wengi wa waungaji mkono wa waasi wanadai kuwekwa zoni moja ama zaidi za kutoruka ndege katika anga ya Syria kuwalinda wapinzani na kuwaruhusu kuunda serikali mbadala katika ardhi ya Syria ambayo inaweza kuomba usaidizi zaidi wa kijeshi wa kuingilia kati kutoka mataifa ya magharibi pamoja na washirika wa Kiarabu.

Baada ya siku nane za mivutano ya kutaka udhibiti na kwamba hakuna mshindi wa wazi, upinzani nchini Syria unaonekana kuwa umegawika zaidi kuliko hapo kabla.

Waasi wapoteza imani

Ndani nchini Syria, waasi wanaopigana na utawala wa rais Bashar al-Assad na wanaharakati wanasema kuwa wamepoteza uaminifu kwa wapinzani wanaoishi uhamishoni ambao wanaonekana kuwa hawana uwezo wa kuzuwia jeshi ya serikali kusonga mbele.

Muungano wa kitaifa umekamilisha mkutano wake uliodumu kwa siku kadha nchini Uturuki siku ya Ijumaa ambapo ulishuhudia waasi kutoka Qatar na Saudi Arabia wakifikia muafaka dakika za mwisho hali iliyofikiwa kwa upatanishi chini ya mbinyo mkubwa.

Baada ya saa kadha za mivutano , mkuu wa muungano huo George Sabra alitangaza kupanuliwa kwa kundi hilo na kujumuisha wajumbe 51 wengine wapya,na kufikisha idadi ya wajumbe 114.

George Sabra, the new head of the main Syrian opposition bloc in exile, the Syrian National Council, speaks to reporters during a press conference on the sidelines of the General Assembly of the Syrian National Council meeting in Doha,on November 10, 2012. Sabra struck a combative tone, saying international inaction rather than divisions among anti-regime groups are to blame for the inability to end the bloodshed in Syria. AFP PHOTO/KARIM JAAFAR ==QATAR OUT == (Photo credit should read KARIM JAAFAR/AFP/Getty Images)
Mkuu wa muungano wa kitaifa George SabraPicha: KARIM JAAFAR/AFP/Getty Images

Hadi sasa muungano huo umekuwa na wajumbe wengi kutoka kundi la udugu wa Kiislamu linaloungwa mkono na Qatar , lakini Saudi Arabia ambayo ina nguvu katika eneo hilo inataka kupunguza ushawishi huo.

Kati ya wajumbe hao wapya , kiasi ya 10 wanahusika na mpinzani maarufu Michel Kilo, ambaye juhudi zake za kuingia katika muungano huo ziliungwa mkono na Saudi Arabia.

epa03711995 US Secretary of State John Kerry (L) speaks during a press conference with Jordanian Foreign Minister Nasser Judeh (R) in Amman, Jordan, 22 May 2013. Key members of the Friends of Syria group are meeting in Jordan with the aim of laying the groundwork for talks to bring about an end to the Syrian conflict. Foreign ministers of the United States, Britain, France, Saudi Arabia, Qatar, Turkey, Jordan, the United Arab Emirates, Egypt, Germany and Italy were gathering in Amman. EPA/JAMAL NASRALLAH
Waziri John KerryPicha: picture alliance / dpa

Urusi yaonywa

Wakati huo huo Ujerumani na Marekani zimeionya Urusi jana Ijumaa(31.05.2013) kutohatarisha mkutano uliopangwa kwa ajili ya amani ya Syria ama kubadilisha uwiano wa nguvu katika mashariki ya kati kwa kuupatia utawala wa rais Bashar al-Assad silaha za kisasa za ulinzi wa anga.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na waziri mwenzake wa Ujerumani Guido Westerwelle wamesema kupeleka makombora ya S-300 kutoka Urusi kwenda Syria kutarefusha vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe, kuzuwia juhudi za kuunda serikali ya mpito kwa njia ya mazungumzo na kuathiri maslahi ya Israel ya kimkakati.

U.S. Secretary of State John Kerry (R) meets with Israeli President Shimon Peres in Jerusalem, May 23, 2013. REUTERS/Jim Young (JERUSALEM - Tags: POLITICS)
Kerry akizungumza na rais wa Israel ShimonPicha: Reuters

Kerry amewaambia waandishi habari katika mkutano wa pamoja na Westerwelle baada ya mkutano wao katika wizara ya mambo ya kigeni. "Tunawaomba tena kutoathiri uwiano katika eneo hilo kwa mtazamo wa Israel," amesema. "silaha ambazo zitapelekwa kwa Assad hata kama ni mkataba wa zamani ama vinginevyo, una athari mbaya katika uwiano wa maslahi na uthabiti wa eneo lote na unaiweka Israel katika hali mbaya.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / afpe / ips

Mhariri : Bruce Amani