1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wajongelea Tripoli

21 Agosti 2011

Waasi wa Libya wamesonga mbele kuelekea katika mji mkuu Tripoli, jumamosi usiku, huku utawala wa Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ukionekana kumong'onyoka.

https://p.dw.com/p/12KlN
Wapiganaji waasi wakishangilia baada ya kufika BregaPicha: dapd

Ripoti zinasema kuna mapigano makali ya bunduki na miripuko katika viunga vya mjio huo mkuu.

Sasa waasi wanadai kuwa wameudhibti mji muhimu wa bandari wa Brega. Kwa kuuteka mji huo, waasi wataweza kudhibiti vituo muhimu vya mafuta, ikiwa ni pamoja na kituo cha kusafishia mafuta katika mji wa Zawiya waliouteka siku mbili zilizopita.

Hapo jana kiongozi wa waasi nchini humo, Mustafa Abdel Jalil alisema, mwisho wa Gaddafi unakaribia. Gaddafi ametawala Libya kwa miaka 41.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri Prema Martin