1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wasonga mbele nchini Libya

28 Machi 2011

Mapigano yanaendelea nchini Libya, ambapo vikosi vya waasi nchini humo vinadaiwa kusonga mbele na kuirejesha miji kadhaa iliyokuwa inashikiliwa na vikosi vinavyoumuunga mkono Kiongozi wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/10j2F
Waasi wa Libya wakishangilia ushindiPicha: AP

Hatua hiyo inatokana na vikosi vya Gaddafi kusambaratishwa na makombora ya anga yanayofyatuliwa na vikosi vya Muungano.

Hivi sasa mapigano kati ya waasi na vikosi vya serikali yanafanyika karibu na eneo analotoka Kiongozi wa Libya Muammar Gaddaf, mjii wa Sirte, huku kukiwa na taarifa zisizo rasmi za waasi hao kuushikilia mji huo.

Sauti kubwa za milio minane tofauti ya makombora imesikika, ikitajwa kuwalenga waasi hao ambao wameonekana kuingia katika eneo la mji huo.

Sirte ni mji uliyopo umbali wa kilometa 360, mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli.

Taarifa kutoka katika uwanja wa mapigano zinasema kwamba waasi tayari wameuteka mji wa Bin Jawad, baada ya kufanikiwa kufanya hivyo katika mji mwingine wenye utajiri mkubwa wa mafuta wa Ras Lanuf.

Waasi hao ambao walipoteza muelekeo katika mapambano wiki mbili zilizopita, hivi sasa wanasonga mbele kwa msaada wa majeshi ya Muungano ambayo yamekuwa yakivisamabratisha vikosi vya Gadaffi kwa makombora yake ya kutoka angani.

Mashahidi wamesema mapema leo vikosi vya waasi vikiwa na magari yaliyobeba silaha kali na nzito yalionekana yakielekea mji huo wa kiongozi wa Libya wa Sirte.

Asubuhi ya leo katika mitaa ya mji huo, wenye jumla ya watu wanakodiriwa kufikia 1,20,000, kulikuwa kimya kabisa na hakukuwa na ishara yeyote kwamba miripuko iliyotoke usiku wa kuamkia leo imesababisha athari zozote kwa umma.

Taarifa hizo kutoka katika maeneo kadhaa ya mji huo, zinaeleza kuwa bado mji huo upo chini ya vikosi vya Gaddafi ambavyo vimeonekana vikifanya doria katika mitaa kadhaa.

Walioshuhudia wamesema wanajeshi wanaounga mkono kiongozi huyo wameoneakana wakiwa katika gari ndogo za kiraia na nyingine za kijeshi zilizibeba silaha.

Awali upande wa waasi ulitoa taarifa za kwamba mji wa Sirte upo katika himaya yao, jambo ambalo mpaka sasa halijathibitishwa.

Msemaji wa waasi, Shamsiddin Abdulmolah, alijigamba kuwa vikosi vyao havikupata upinzani wowote kutoka kwa vikosi vya Gaddafi, wakati taarifa za ndani ya mji wa Sirte zinasema mpaka sasa bado vikosi vya Gaddafi vinatawala.

Hata hivyo, kumeonekana magari takribani 20 ya Kijeshi yakiwa na silaha nzito pamoja magari mengine ya kiraia yakiondoka mjini Sirte kuelekea Tripoli.

Mashambulizi ya vikosi vya Muungano yanadaiwa yamesababisha vifo vya raia, ingawa Wazri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, anakanusha.

Israel USA Verteidigungsminister Robert Gates bei Benjamin Netanyahu in Caesarea
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert GatesPicha: AP

"Lakini tuna taarifa za kiinterijensia kwamba Gaddafi anachuka miili ya watu aliowauna na kuiweka katika eneo tulilofanya mashambulizi,tunachukua tahadahri ya hali ya juu katika jitihada ya kijeshi."

Qatar leo imekuwa nchi ya pili kulitambua Baraza la Waasi nchini Libya kama chombo kinachowakilisha wananchi baada ya Ufaransa, wakati huu waasi hao wakijiandaa kuunda serikali ya muda

Kwa ujumla, mpaka sasa Waasi wanashikilia maeneo muhimu yenye hazina ya mafuta ya Es Sider,Ras Lanuf, Brega, Zuetina na Tobruk wakati Gaddafi akishikilia maeneo ya mashariki.,

Mwandishi:Sudi Mnette //RTRE/AFP

Mhariri: Miraji Othman