1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau wajadili vita dhidi ya ujangili

Admin.WagnerD13 Februari 2014

Mkutano wa Kimataifa juu ya Ujangili unafanyika mjini London huku viongozi wanne wa Afrika akiwemo Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wakiwa miongoni mwa wakuu 40 wa nchi waliohudhuria.

https://p.dw.com/p/1B7um
Mwanamfalme William, muandaji wa mkutano wa kupiga vita ujangili.
Mwanamfalme William, muandaji wa mkutano wa kupiga vita ujangili.Picha: Reuters

Mkutano huo unafanyika wakati Mwanamfalme William wa Uingereza akitoa wito wa kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu na vifaru akisema ni biashara isiostahili kwa wanyama hao.

Wawakilishi wa mataifa takriban 50 wamekusanyika mjini London kwa mazungumzo hayo yanayonuiwa kutekelezwa kwa sheria juu ya ujangili hasa katika Mataifa mengi ya Afrika ambako ujangili huo unafanyika kwa kiasi kikubwa na kupata biashara katika masoko ya Asia. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Uingereza na mwanamfalme Charles na William wameuita mkutano huo kuwa muamko mzuri katika vita dhidi ya Ujangili.

Pembe za ndovu na faru zilizokamatwa nchini Zimbabwe.
Pembe za ndovu na faru zilizokamatwa nchini Zimbabwe.Picha: Desmond Kwande/AFP/Getty Images

"Leo hii tuko hapa tukiwa na lengo moja, kutumia ushawishi wetu wa pamoja kusimamisha mauaji na usafirishaji haramu wa pembe za baadhi ya wanyama wanaoenziwa duniani na walio hatarini kutoweka," Alise wanamfalme William katika hotuba yake kwa wageni waalikwa katika sherehe iliofanyika jana jioni.

Mkutano wa kwanza wa aina yake

Mwanamfalme huyo alisema hakujawahi kuwepo na mkusanyiko wa kikundi kikubwa ambacho nia yao ni kupinga ujangili huku akisema kuwa ni wajibu wa kila mmoja katika kundi hilo kuhakikisha tarehe 13 mwezi wa Februari mwanzo wa kumaliza visa visivyaostahili vya biashara haramu ya pembe za wanyama.

Kulingana na makadirio yalio rasmi takriban ndovu 25,000 wanauwawa kila mwaka na majangili huku Afrika kusini ikipoteza vifaru 1000 mwaka uliopita ikilinganishwa na vifaru 13 waliopotea mwaka wa 2007.

Hata hivyo mataifa ya Afrika ya kati yanasemekana kuwa katika hali mbaya zaidi ambapo Gabon ndio nchi inayopoteza wanyama wake kwa wingi na kupata hasara kubwa. Hatua hii ya kuongezeka kwa ujangili inasemekana kushamirin kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara matajiri wa eneo la Asia wanaotumia pembe za vifaru na ngozi ya chui kama dawa za kiasilia huku pembe za ndovu zikitumika kutengeneza mapambo.

Faru wako hatarini kutoweka kutokana na kuwindwa kwa ajili ya pembe zao.
Faru wako hatarini kutoweka kutokana na kuwindwa kwa ajili ya pembe zao.Picha: ALEXANDER JOE/AFP/Getty Images

Ghali kuliko dhahabu

Kwa sasa pembe moja ya kifaru inagharibu dola 60,000 sawa na euro 44,000 ikiwa ni kiwango kikubwa cha fedha ikilinganishwa na bei ya dhahabu au hata madawa ya kulevya aina ya cocaine.

Naibu Wazirir wa Mazingira wa China Zhang Jianlong atakuwepo katikamkutano huo pamoja na Viongozi wa nne wa nchi za Afrika za Chad, Gabon, Botswana na Tanzania. Mwanamfalme Charles na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron pia watahudhuria mkutano huo pamoja na Mwanamfalme William ambaye katika siku za hivi karibuni alikosolewa baada ya kuonekana akiwinda nguruwe mwitu.

Aidha Mcheza filamu mashuhuri Jackie Chan na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa China wa mchezo wa mpira wa vikapu kwa wanaume Yao Ming wanatarajiwa lkuiunga mkono kampeni ya kupiga vita ujangili kwa kutoa ujumbe wa video katika mkutano huo wa leo.

Mwandishi: Amina Abubakar/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman