1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC watiwa mbaroni nchini Zimbabwe

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxf

Harare

Polisi nchini Zimbabwe wanasema wanachama 200 wa upande wa upinzani waliokamatwa jana-wanatuhumiwa kua nyuma ya mashambulio ya hivi karibuni ya mabomu ya mikono dhidi ya polisi,maduka na wafuasi wa serikali.Chama cha upinzani cha MDC kinahisi tuhuma hizo zimelengwa kuhalalisha visa vya ukandamizaji kabla ya uchaguzi wa bunge hapo mwakani.Msemaji wa chama cha upinzani cha MDC Nelson Chamisa alisema hapo awali polisi imeyavamia makao makuu ya chama chao mjini Harare na kuwakamata zaidi ya watu 200.Hakutoa sababu ya kukamatwa kwao.Kwa upande wake msemaji wa polisi,Andrew Phiri ameviambia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali kwamba wafuasi waliokamatwa wa MDC wanatuhumiwa kuhusika na kampeni ya mashambulio ya mabomu na watafikishwa mahakamani hivi karibuni.”