1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Waserbia wa Kosovo waondoa vizuizi vilivyozusha mvutano

29 Desemba 2022

Rais wa Kosovo Aleksandar Vucic amesema Waserbia wa Kosovo ambao wamekuwa wakifunga barabara kwa karibu wiki tatu watabomoa vizuizi vyao.

https://p.dw.com/p/4LWhP
Kosovo Metrovica Straßenblockade
Picha: Vudi Xhymshiti/AA/picture alliance

Kauli hii ni kufuatia wito wa Marekani na Ubelgiji unaohimiza kupunguza mvutano katika eneo hilo linalokabiliwa na hali tete.

"Vizuizi vitaondolewa, lakini kutoaminiana kunabaki," alinukuliwa rais Vucic na shirika la utangazaji la serikali la RTS jana Jumatano wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa Waserbia wa Kosovo karibu na mpaka.

soma Kosovo yafunga mpaka wake na Serbia kufuatia maandamano

Vucic amesema "Huu sio mchakato rahisi, na hauwezi kutekelzwa kwa masaa mawili, kama wengine walivyofikiria. Lakini ndani ya saa 24 hadi 48 vizuizi vitaondolewa. ila hali ya kutoaminiana haiondoki. Wale ambao wanapuuza uwepo wa Waserbia huko Kosovo lazima wajue kwamba, kama ambavyo haturuhusu sasa,basi hatutaruhusu katika siku zijazo pia."

Kosovo ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Serbia mwaka 2008, lakini Belgrade imekataa kuitambua na kuwahimiza Waserbia 120,000 wa Kosovo kukaidi mamlaka ya Pristina hasa kaskazini ambako Waserbia asili ndio wengi.

soma Serbia yaionya NATO juu ya usalama wa waSerbia walioko Kosovo

Mzozo upya

Kosovo | ethnische Spannungen vor den Kommunalwahlen
Picha: Bojan Slavkovic/AP Photo/picture alliance

Matatizo ya hivi punde yalizuka mnamo Desemba 10, wakati kabila la Waserbia lilipoweka vizuizi kupinga kukamatwa kwa polisi wa zamani anayeshukiwa kuhusika katika mashambulizi dhidi ya maafisa wa polisi wa kabila la Albania na kwa ufanisi kuziba barabara kwenye vivuko viwili vya mpaka.

Baada ya vizuizi hivyo kuwekwa, polisi wa Kosovar na walinzi wa amani wa kimataifa walishambuliwa katika matukio kadhaa ya ufyatulianaji risasi, huku vikosi vya kijeshi vya Serbia vikiwekwa katika hali ya tahadhari wiki hii.

Umoja wa Ulaya na Marekani zilielezea wasiwasi wao kuhusu hali hiyo, na kuhimiza kusitishwa kwake mara moja na kusema kuwa wanafanya kazi na viongozi wa Serbia na Kosovo kutafuta suluhu ya kisiasa kwa moja ya mizozo mibaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka kadhaa kaskazini mwa Kosovo.

Urusi ambayo ni mshirika wa Belgrade imetoa sauti kuunga mkono Serbia na kusema kuwa inafuatilia kwa karubu sana matukio hayo huku Ujerumani ikionya dhidi ya kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi karibu na mpaka wa Kosovo.

Umoja wa Ulaya na mabalozi kadhaa wa kimataifa wiki hii wamelaani mashambulizi manne ya hivi majuzi dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakiandika habari kuhusu tukio hilo.