1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasudan wa kusini na kaskazini wapambana

10 Oktoba 2010

Nchini Sudan,polisi walitumia marungu kuwatawanya kiasi ya waandamanaji 30 waliokuwa wakidai uhuru wa eneo la kusini.

https://p.dw.com/p/PaPh
Southern Sudan President and elections candidate Salva Kiir waits to casts one of his ballots at a poling station set in a restaurant in Juba, southern Sudan, Sunday April 11, 2010. The people of Southern Sudan will cast ballots in a national election for the first time in more than two decades as a three-day election begins Sunday. Despite the first-in-a-generation vote, most people are already looking past the elections to a vote next January considered far more significant: a referendum on independence that could signal the birth of a new African nation, if final negotiations with Khartoum over oil rights and the location of the border are worked out peacefully. (AP Photo/Jerome Delay)
Rais wa kusini ya Sudan, Salva Kiir.Picha: AP

Waandamanaji hao walitoa mwito huo kwenye mkutano ulioitishwa na serikali kuunga mkono umoja wa taifa katika mji mkuu Khartoum. Kiasi ya watu 3,000 walikusanyika karibu na makao rasmi ya rais kwa mkutano huo,hivi sasa ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kupigwa kura ya maoni. Katika kura hiyo wakaazi wa kusini ya Sudan wataamua iwapo eneo hilo la kusini linataka kujitenga au kubakia sehemu ya Sudan iliyoungana.

United Nations Ambassador-designate Susan Rice listens as President-elect Barack Obama, not pictured, announces his national security team at a news conference in Chicago, Monday, Dec. 1, 2008. (AP Photo/Charles Dharapak)
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice.Picha: AP

Mkutano huo umefanywa mjini Khartoum, wakati ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulioongozwa na balozi wa Marekani Susan Rice ulikuwa ukikamilisha ziara yake ya siku nne nchini Sudan. Hali ya mvutano imezidi kati ya kaskazini na kusini ya Sudan kabla ya kupigwa kura ya maoni tarehe 9 Januari.