1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 44 wauwawa Nigeria

24 Agosti 2013

Watu wanaodhaniwa kuwa ni waislamu wenye itikadi kali wameshambulia kijiji na kuwauwa watu 44 huko kaskazini mashariki mwa Nigeria mapema wiki hii.(24.08.2013)

https://p.dw.com/p/19VVd
This picture taken on April 30, 2013 shows a Nigerian soldier, part of the 'Operation Flush' patrolling in the remote northeast town of Baga, Borno State. Nigeria's military said on May 16, 2013 that it was ready to launch air strikes against Boko Haram Islamists as several thousand troops moved to the remote northeast to retake territory seized by the insurgents. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images)
Nigeria Kampf gegen Boko Haram IslamistenPicha: Getty Images/AFP

Taarifa zinasema unyama huo umefanyika katika kijiji cha Demba kilichopo karibu na mji wa Baga kaskazini mwa jimbo la Borno, sehemu iliyokuwa ngome ya kundi la Boko Haram kabla ya kusambaratishwa na jeshi katikati ya mwezi Mei. Kitendo hicho kiliwafanya wanamgambo wa kundi hilo kukimbilia mafichoni au kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Cameroon.

Kuchelewa kwa taarifa za mauwaji

Shambuzili limeelezwa kufanyaka Jumatatu lakini taarifa zake zimeibuka hivi karibuni kutokana na eneo hilo kuwa katika maeneo ya vijijini sana na kwamba mawasiliano ya simu yalikatwa na serikali kwa lengo la kuvuruga operesheni za Boko Haram.

Soldiers walk on April 30, 2013 in the street in the remote northeast town of Baga, Borno State. Fierce fighting between Nigerian troops and suspected Islamist insurgents, Boko Haram at Baga town in the restive northeastern Nigeria, on April 25, 2013 left dozens of people dead and scores of civilians injured. But the military denied the casualty figures claiming it was exaggerated to smear its image. Meanwhile normalcy has return to the town as residents are going about their normal business. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images)
Mji wa Baga, jimbo la Borno NigeriaPicha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Kundi hilo linataka kuwepo kwa sheria za Kiislamu katika eneo la pamoja na vikundi vingine vya Waislamu ambavyo vilikuwa kitisho kikubwa cha usalama wa Nigeria.

Baadhi ya raia wamechinjwa

Mmoja kati ya wafanyakazi wa huduma ya dharura katika eneo hilo aliyezungumza na shirika la habari la reuters kwa masharti ya kutotajwa jina lake kwa kuhofia usalama wake, alisema walichoma moto nyumba, kupiga risasi watu, na kuwachinja watu. Maafisa wa usalama katika maeneo hayo wamethibitisha kutokea vifo hivyo.

Shumbulio hilo limefanyika siku ambayo serikali pia ilitangaza kuwa mmoja kati ya viongozi muhimu wa Boko Haram, Aboubakar Sheka atakuwa ameuwawa kati ya Julai 25 na Agosti 4, kutoka na jeraha alililolipata baada ya kutokea mapigano kati ya kundi hilo na vikosi vya usalama vya serikali.

Tangazo la Mauwaji na kifo cha kiongozi wa Boko Haram

Madai ya kifo cha kiongozi huyo yametajwa kulipunguza nguvu kundi hilo lakini pia uwezo wa kutekeleza operesheni zake unaonekana kupungua tangu rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kutangaza hali ya hatari huko kaskazini mwa Nigeria, katika majimbo matatu yaliyoathirika vibaya zaidi na kuanzisha rasmi mpango maalumu wa kulisambaratisha mwezi Mei mwaka huu.

Baga ni mji ulioshuhudia mapigano yaliyojumuisha wanajeshi wa Nigeria, Chad na Niger na wanamgambo wa Kiislamu mwezi Aprili ambayo yalisababisha vifo vya idadi kubwa ya watu. Jeshi lilisema watu 37 waliuwawa lakini viongozi wa mji huo walisema kaasi watu 185, wengi wao wakiwa raia wasio na hatia waliuwawa katika vurugu hizo.

Jeshi lilisema Boko Haram waliwauwa watu wengine 20 katika mji huo mwezi uliopita. Nigeria taifa lenye zaidi ya watu milioni 160 barani Afrika limekuwa na migogoro ya kidini ambayo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na Waislamu kwa upande wa kaskazini na Wakristo kusini.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR
Mhariri: Sekione Kitojo