1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani awapa moyo wanajeshi Mali

Sekione Kitojo
31 Julai 2017

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen yuko ziarani  nchini Mali. Yuko mjini Gao kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambako kuna kambi ya wanajeshi wa Ujerumani, wakiwa katika ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/2hQql
Mali Von der Leyen reist nach Mali und Niger
Picha: picture-alliance/dpa/B. Pedersen

Wakisaidia  ulinzi wa  amani  katika  makubaliano ya  amani  yaliyofikiwa  kati  ya serikali  na  waasi. Vikosi  vya Ujerumani  katika  ujumbe  huo vinatumia helikopta  na  ndege zisizo na  rubani. Jumatano  wiki iliyopita  hata  hivyo  helikopta  moja  ilianguka  na  wanajeshi  wawili waliuwawa  katika  ajali  hiyo.

Von der Leyen alikuwa  amepanga ziara  hiyo  muda  mrefu , lakini sasa yumo  katika  maombolezo. Waziri  huyo jana Jumapili  alishiriki  katika  sala ya  kumbukumbu kwa  ajili  ya  wanajeshi  hao katika  kambi ya Castor. Ripoti ya Jens Borchers  kutoka  mjini  Gao inasomwa studioni  na  Sekione Kitojo.

Von der Leyen reist nach Mali und Niger
Waziri Ursula von der Leyen akiwa katika sala ya kumbukumbu ya wanajeshi wawili waliouwawa mjini GaoPicha: picture alliance / Britta Pedersen/dpa

Katika  kambi ya  Castor kumetengenezwa kanisa  la  muda. Kanisa la  martin , hili  sio kanisa  halisi , badala  yake  ni hema tu lililopambwa  kuwa  kanisa  la  muda. Katika  kanisa hilo  kumewekwa mishumaa  pamoja  na  picha  za  wanajeshi  hao  wawili  waliofariki katika  ajali  hiyo  ya  helikopta. 

Akiwa  katika  hali  ya  maombolezi Ursula von der Leyen  aliimba  na  kusali  pamoja  na  kiasi  ya wanajeshi  100  hivi waliofika  katika  sala  hiyo na baadaye aliwahutubia  wanajeshi  hao.

"Kupotelewa huku ni  kugumu sana."

Tangu  miaka  miwili  iliyopita  hakuna mwanajeshi  yoyote  wa Ujerumani  anayeshiriki katika  ulinzi  nje  ya  nchi  ambaye ameuwawa.  Katika  eneo  la  Gao  tumeshuhudia  helikopta  hiyo ikiwa imeanguka  kilometa  70  kaskazini  mwa  mji  huo. Pamoja  na hayo  ni  lazima  wanajeshi  kuendelea  na  shughuli  zao, kulinda eneo  helikopta  hiyo  ilipoanguka na  kupata  taarifa  zaidi.

Bundesverteidigungsministerin Ursula von der Leyen zu Hubschrauberabsturz in Mali
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen Picha: picture alliance/dpa/B. Pedersen

Wasi wasi wa  wanajeshi

Wanajeshi  wengi wanaweza  hapo  baadaye  kuwa  na  wasi  wasi kuhusiana  na  kile  kilichotokea. Ursula von der Leyen  anataka kuzungumza  nao  na  kuwasikiliza.

"Ndio  sababu  nataka  leo kujumuika  na  wanajeshi  na  kutumia muda  kuzungumza  nao."

Ujumbe  huo  wa  wanajeshi  wa  Ujerumani mjini  Gao una wanajeshi 800.  Amesema  mchungaji  anayehudumia  jeshi  hilo wakati  wa  sala  jana  kwamba , wiki  hii  ilikuwa  ngumu  sana kwetu.

Bado hijafahamika bado  ajali  hiyo  ya  helikopta  ilisababishwa  na nini. Kikundi  cha  wataalamu  kimekwisha  wasili  na  kuchunguza chanzo cha  ajali  hiyo. Waziri  amezungumza  na  wataalamu  hao, lakini  matokeo  kamili  bado  hayakuwekwa  wazi. Moja  kati  ya visanduku viwili  vya  kunakili  maelezo  ya  safari  ya  helikopta  hiyo kimepatikana. Kimeharibika, lakini iwapo  taarifa  zitapatikana kutokana  na  kisanduku  hicho, hilo  halijafahamika.

Deutschland Ursula von der Leyen in der Generalfeldmarschall-Rommel-Kaserne
Waziri von der Leyen akizungumza na wanajeshiPicha: picture alliance/dpa/B. Thissen

Lakini  leo  hii  mtazamo  unaelekezwa  katika  mazungumzo na wanajeshi  katika  kikosi  hicho  mjini  Gao.  Von der Leyen hatapendelea  kuzungumzia  tu  kuhusu  kuanguka  kwa  helikopta hiyo.  Anataka  kuwapa  motisha  wanajeshi  hao  na  kuzungumzia nao kuhusu  ujumbe  wao  wa  kulinda  amani  ulio ndani  ya Umoja wa  Mataifa.

Amesema  von der Leyen  kwamba  yuko  nchini  Mali kuwapa  moyo na  kuwaunga  mkono  wanajeshi  hao  kwa  kazi  yao wanayoifanya, na  kwamba  mafanikio  ya  ujumbe  huo  ni  hatua  ya kuhakikisha  usalama  wa  mataifa  jirani. Na  pia  kuimarika kwa mataifa  jirani ya  Ulaya  ni  kuimarika  pia  kwa  Ujerumani  na  pia Ulaya  kwa  jumla.

Mwandishi : Jens Borschers / HR /  Sekione  Kitojo

Mhariri: Yusuf Saumu