1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WIESBADEN: Mkutano wa "Ushirikiano na Afrika"

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AP

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amefungua mkutano kuhusu Bara la Afrika uliopewa jina „Ushirikiano na Afrika.“ Mbali na Rais Köhler,marais wa Msumbiji,Madagaskar,Botswana,Benin na Nigeria ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano huo katika mji mkuu wa jimbo la Hessen,Wiesbaden.Mada kuu zinazojadiliwa na wajumbe 45 ni changamoto za utandawazi,wahamiaji kutoka nchi za Kiafrika na athari za uhamiaji katika nchi za Ulaya zinazofuatwa.