1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WIESBADEN: Sudan yatakiwa ikubali majeshi ya kulinda amani

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN9

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wameitaka Sudan ikubali wanajeshi zaidi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kukisaidia kikosi cha Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur.

Wakimaliza mkutano wao wa siku mbili mjini humo, mawaziri hao wameahidi kushirikiana kijeshi na Umoja wa Mataifa na shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO, kutatua mizozo duniani.

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wameeleza wasiwasi wao juu ya kuzorota kwa hali kibinadamu katika jimbo la Darfur nchini Sudan huku mratibu wa sera za kigeni wa umoja huo, Javier Solana, akimhimiza rais Omar el Bashir wa Sudan akubali majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, aliyekuwa mwenyekiti wa mkutano huo, amesema Umoja wa Ulaya unapanga kuimarisha mipango yake ya kijeshi na operesheni zake ili kuchangia zaidi katika jukumu la usalama wa kimataifa.