1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizi wa mifugo wauwa watu 24 Sudan Kusini

2 Aprili 2024

Watu wasiopungua 24 wameuawa kufuatia mashambulizi ya wezi wa mifugo katika vijiji viwili nchini Sudan Kusini.

https://p.dw.com/p/4eKy6
Mchunga ng'ombe
Mchunga ng'ombe wa kabila la Mundari akiwa na mifugo yake katika eneo la Terekeka, Sudan Kusini.Picha: DW

Mkuu wa kijiji cha Walgak katika jimbo la Jonglei, Simon Gatluak Lam, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba watu wa kabila la Murle walikishambulia kijiji hicho na kuua raia 10, polisi watatu na kuiba karibu ng´ombe 300.

Soma zaidi: Sudan Kusini: Watu 50 wauawa Juba kufuatia mzozo wa mifugo

Baadaye wezi hao walivamia kijiji cha Ajara na kuwaua makumi ya watu, kuwateka nyara watoto wapatao 11 na kuiba ng´ombe na mbuzi kadhaa.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, Sudan Kusini ina takriban ng'ombe milioni 12 na idadi sawa na hiyo ya kondoo na mbuzi.

Makundi hasimu ya kikabila yamekuwa yakishambuliana ili kugombea madaraka na kujinyakulia mifugo.