1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa.Umoja wa Afrika waishutumu Sudan na Janjaweed.

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrQ

Umoja wa Afrika umeishutumu serikali ya Sudan pamoja na wanamgambo wa Janjaweed kwa kufanya mashambulizi mapya katika jimbo la Darfur.

Umoja wa Afrika , ambao wanajeshi wake 7,000 wanaangalia hali ilivyo katika jimbo hilo lililokumbwa na machafuko, umesema mashambulizi ya anga na ardhini ya jeshi hilo pamoja na wanamgambo hao yamesababisha raia kadha kuuwawa na wengine kujeruhiwa.

Maafisa wa umoja wa Afrika wamesema kuwa mashambulizi hayo ni uendeaji kinyume dhahiri wa makubaliano ya kimsingi ya amani kwa ajili ya jimbo la Darfur.

Akizungumza mjini Khartoum baada ya shutuma hizo kujitokeza , mkuu wa huduma za kiutu wa umoja wa mataifa Jan Egeland ameitaka serikali ya Sudan kufanyakazi pamoja na umoja wa mataifa kusitisha mateso hayo kwa watu wa Darfur.

Hakuna jibu kutoka Khartoum hadi sasa.

Zaidi ya watu 200,000 wameuwawa na zaidi ya wengine milioni nne wamelazimika kuyakimbia makaazi yao katika muda wa miaka mitatu ya mapigano.