1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yapokea uenyekiti wa G20

10 Septemba 2023

India imekabidhi rasmi uenyekiti wa mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi G20, kwa Brazil katika hafla ya kufunga mkutano wa kilele wa kila mwaka.

https://p.dw.com/p/4WA6n
Indien | G20-Gipfel | Narendra Modi und Luiz Inacio Lula da Silva
Narendra Modi na Luiz Inacio Lula da SilvaPicha: AFP

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amekamilisha kipindi chake na kukabidhi uenyekiti huo wa kupokezana kwa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.

Soma pia: Viongozi wa kundi la G20 wanaokutana nchini India, wamekubaliana kutoa tamko la pamoja linaloepuka kuilaani Urusi

Baada ya kupokea kiti hicho, Lula amesema kuwa  "masuala ya kijiografia ya kisiasa" hayapaswi kukwamisha majadiliano ya G20, akimaanisha malumbano ya kidiplomasia kuhusu vita vya Ukraine.

Viongozi wa G20 wamekuwa na mvutano mkubwa juu ya vita hivyo, tangu vilipoanza mwaka jana, huku Rais wa UrusiVladimir Putin akikosa kuhudhuria mkutano huo ili kukwepa mzozo wa kisiasa.