1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon: Jenerali Nguema ateua wapinzani kuongoza serikali

12 Septemba 2023

Kiongozi mpya wa Gabon, Brice Oligui Nguema amemteua kiongozi wa upinzani Paulette Missambo kuwa kiongozi wa Bunge la seneti.

https://p.dw.com/p/4WF1g
Kiongozi wa mpito Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema
Kiongozi wa mpito Gabon Jenerali Brice Oligui NguemaPicha: AFP/Getty Images

Wakati huo huo, Nguema amemteua Jean Francois Ndongou, aliyeshikilia nyadhifa mbalimbali za uwaziri chini ya utawala wa Bongo, kuwa spika wa bunge la kitaifa.

Nguema, aliyetangazwa kuwa rais wa mpito, aliongoza mapinduzi yasiyo na umwagaji damu yaliyomuondoa madarakani Ali Bongo Ondimba mnamo Agosti 30.

Soma pia:Utawala wa kijeshi Gabon wamemteua kiongozi wa upinzani kuwa Waziri Mkuu wa mpito

Jenerali huyo wa jeshi ameahidi kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia na kufanyika kwa uchaguzi baada ya kipindi cha mpito japo hakuweza wazi tarehe maalum ya hilo kufanyika.

Tayari ameunda serikali ya mpito chini ya waziri mkuu mpya Raymond Ndong Sima, mchumi aliyesoma nchini Ufaransa na aliyewahi kuhudumu kama waziri mkuu chini ya utawala wa Bongokutoka mwaka 2012 hadi 2014 kabla ya kushindana naye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 na 2023.