1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya yatafautiana juu ya suala la Uturuki

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkG

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wako mjini Brussels nchini Ubelgiji kujaribu kufikia makubaliano ya jinsi ya kusonga mbele na harakati za Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Waziri wa mambo ya nje ya Ujerumani Frank Walter Steinmeir amesema kwamba msimamo wa nchi za Umoja wa Ulaya unatafautiana sana juu ya namna Uturuki inavyopaswa kuadhibiwa kutokana na kushindwa kufunguwa bandari zake zote na viwanja vya ndege kwa Cyprus nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Tume ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza usitishaji wa muda wa mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo.Viongozi wa serikali za Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Brussels hapo Alhamisi na Ijumaa na suala la uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Uturuki linatazamiwa kupewa kipau mbele kwenye agenda.