1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Uturuki lakiri marufuku ya hijab yaondolewe

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4yI

Ankara:

Bunge la Uturuki limeidhinisha awamu ya kwanza kati ya mbili za mageuzi ya katiba,yenye lengo la kuondowa marufuku ya wasichana kufunga hijab katika vyuo vikuu nchini humo.Wabunge wa chama tawala cha AKP na wenzao wa chama cha nadharia kali za kizalendo-wameunga mkono kwa pamoja mageuzi hayo marekebisho hayo ya katiba.Serikali ya waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan inasema marufuku ya kufunga hijab yanawanyima wakina mama haki ya kusoma katika vyuo vikuu.Lakini jumuia za wasiopendelea shughuli za kidini ziingilie mambo ya serikali,ikiwa ni pamoja na wasomi,wanaamini uamuzi wa kuwaruhusu wakinamama wafunge hijab ni hatua ya mwanzo tuu katika juhudi za kurejesha dini katika maisha ya kijamii nchini humo.Maelfu ya waturuki wameteremka majiani mjini Ankara hii leo kulalamika dhidi ya kuondolewa marufuku ya kufunga hijab.