1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watakaomtukana rais watachukuliwa hatua Tanzania

Amina Mjahid
23 Julai 2019

Chama cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania kimesema kitawachukulia hatua za kinadhamu viongozi na wanachama wote watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwemo vitendo vya kumtukana na kumdhalilisha Raisi wa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/3Maoc
Tansania Daressalam Präsident John Magufuli
Picha: DW/E. Boniphace

Kauli hiyo kali imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM taifa Dr Bashiru Ally mjini Dodoma wakati akihutubia katika shughuli ya uzinduzi wa miradi ya CCM.

Dr Bashiru amesema kumezuka tabia ya ajabu kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kutoa maneno ya matusi na kejeli kwa Raisi wa Tanzania John Magufuli bila hata kujali juhudi kubwa za kuleta maendeleo zinazofanywa na chama hicho.

Katibu Mkuu huiyo wa CCM ameongeza kuwa CCM haitawafumbia macho baadhi ya viongozi ambao wamekuwa na tabia aliyoiita ya kipumbavu ya kuonesha usaliti na matusi ya wazi wazi kwa Raisi Magufuli na kuongeza kuwa CCM haina mpasuko wowote isipokuwa kuna baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho amabao hata hivyo hakuwataja majina yao kuwa ni walafi na wabinafsi na wasioitakia mema Tanzania.

Wahlkampf Tansania
Wafuasi wa Chama tawala cha Mapinduzi CCM nchini TanzaniaPicha: DW

Je kuna mpasuko ndani ya chama tawala?

Siku za hivi karibuni kumekuwepo na sitofahamu ndani ya CCM hadi kupelekea wadadisi wa masuala ya siasa nchini Tanzania kusema kuwa kunaonekana kuwepo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Hali hiyoinafuatia makatibu wakuu wasitafu wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Yusufu Makamba na Abdulrahman Kinana, kutoa waraka kwenda kwa baraza la Wazee wa chama hicho wakilalamika kuchafuliwa katika mitandao ya kijamii, na vyombo vya habari na Bwana Siprian Musiba anayejiita mwananharaki huru.

Hata hivyo wakati waraka wa makatibu wakuu hao wasitafu wa CCM ukiendelea kuzua kizungumkuti, kumekuwepo na kudukuliwa kwa sauti zinazosemekana ni za baadhii ya viongozi na wanachama wa CCM kukisika wakimtukana Rais Magufuli na kuonyesha kutokubaliana naye katika harakati zake za kuleta maendeleo nchini Tanzania.