1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Wanajeshi Mali,Wagner wamefanya mauaji ya raia kiholela

Tatu Karema
25 Julai 2023

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema jeshi la Mali na kundi la mamruki wa kijeshi la Urusi Wagner, wamefanya mauaji ya kiholela, uporaji, kupoteza watu kwa lazima na unyanyasaji mwingine.

https://p.dw.com/p/4ULNt
Human Rights Watch - Jose Miguel Vivanco
Picha: Irene Valiente/EFE/dpa/picture alliance

Human Rights Watch imesema ukatili huo ulitokea katika eneo la kati nchini Mali na kwamba raia kadhaa waliuawa kiholela ama kupotezwa tangu Desemba 2022. 

Kundi hilo liliwahoji watu 40 kwa njia ya simu, wakiwemo mashahidi, na kukagua vidio iliyoonesha ushahidi wa dhuluma zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi hao wa Mali na washirika wao wa kigeni.

Soma pia:Guterres awasilisha ajenda mpya ya amani ya ulimwengu

Kwa kujibu madai hayo ya Human Rights Watch, wizara ya mambo ya nje ya Mali imesema haifahamu kuhusu unyanyasaji huo na kwamba uchunguzi utaanzishwa.