1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon ziarani Burundi

20 Oktoba 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Brice Oligui Nguema, anatarajiwa kuwasili nchini Burundi katika juhudi za kusaka uungwaji mkono na mataifa mengine ya Kiafrika baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4Xmuu
Gabun, Libreville | General Brice Oligui Nguema wird als Interimspräsident vereidigt
Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Brice Oligui Nguema.Picha: AFP/Getty Images

Ziara hiyo inayoanza Ijumaa (Oktoba 20) ina lengo la kukutana na viongozi wakuu wa Burundi akiwemo mwenyeji wake, Rais Evariste Ndayishimiye, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Soma zaidi: Kiongozi wa kijeshi Gabon ateuwa wabunge wapya wa Bunge la Kitaifa

Tangu kumuondowa madarakani Omar Ali Bongo, Nguema amezuru mataifa kadhaa hasa katika ukanda wa Afrika ya Kati kutafuta uungwaji mkono kwa jitihada za utawala wake unaotaka vikwazo vilivyowekwa dhidi yake viondolewe.

Soma zaidi: Brice Oligui Nguema ateua wapinzani kuongoza Bunge

Jumuiya ya kimataifa ililaani mapinduzi ya Agosti 30 mwaka huu yaliyomuondowa madarakani Bongo, ambaye familia yake ilikuwa imeitawala Gabon kwa zaidi ya miaka 55.