1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi Gabon ateuwa wabunge wapya wa kitaifa

7 Oktoba 2023

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema leo ameteuwa wabunge wa Bunge jipya la Kitaifa na Seneti kwa kipindi cha mpito kabla ya uchaguzi ulioahidiwa katika tarehe isiyojulikana.

https://p.dw.com/p/4XFFE
Gabun, Libreville | General Brice Oligui Nguema wird als Interimspräsident vereidigt
Kiongozi wa kijeshi Gabon jenerali Brice Oligui NguemaPicha: AFP/Getty Images

Kiongozi huyo ametua majina 98 ya wabunge wapya wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani na baadhi ya waliomuunga mkono rais aliyepinduliwa Ali Bongo Ondimba.

Jeshi lilikuwa tayarilimeunda serikali ya kiraiakwa kipindi cha mpito iliyoongozwa na Raymond Ndong Sima kama waziri mkuu. Sima aliwahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya kuwa mwanasiasa mkuu wa upinzani chini ya utawala wa Bongo.

Soma pia:Brice Oligui Nguema ateua wapinzani kuongoza Bunge

Wakuu wa jeshi na polisi waliungana Agosti 30 kufanya mapinduzi yasiyo na umwagaji damu yaliyoungwa mkono na wanasiasa, mashirika ya kiraia na umma baada ya zaidi ya miaka 55 ya utawala wa familia ya Bongo.