1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi linalohimiza maendeleo kwa Afrika lakutana na Merkel.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdjU

Berlin.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekutana jana na kundi linalohimiza maendeleo ya Afrika kujadili njia ya kuendeleza kasi hiyo ya ukuaji kabla ya Ujerumani kukabidhi urais wa kundi la mataifa tajiri G8 kwa Japan. Chini ya uongozi wa Ujerumani , mataifa ya G8 mwaka huu yaliamua kusisitiza jukumu lao la kuliondoa bara la Afrika kutoka katika umasikini.

Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan amesema kuwa maendeleo ya kiuchumi yanatokea hivi sasa katika bara hilo.

Annan amesisitiza kuwa bara la Afrika hivi sasa liko katika hatua ya kuchipuka.

Amempongeza kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa uongozi wake katika kundi hilo la mataifa tajiri.

Annan amesema kuwa jopo la maendeleo kwa Afrika lililoundwa mwaka 2005 kuangalia utekelezajki wa ahadi zilizotolewa kwa Afrika , pia linatarajia kuwa serikali za mataifa ya Afrika kutekeleza majukumu yake juu ya utawala bora na haja ya kupambana na rushwa.