1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kwanini Marekani inachukua hadhari kuipatia Ukraine silaha?

12 Aprili 2023

Marekani inaitumia Ukraine silaha huku kukiwa na udhibiti wa utumiaji wa silaha hizo. Wachambuzi wanasema Marekani inafanya hivyo ikijaribu kuepuka mvutano na Urusi.

https://p.dw.com/p/4PxXE
Mizinga ya Howitzers
Mizinga ya HowitzersPicha: Serbian Defense Ministry Press /AP/picture alliance

Kuanzia vifaru chapa Leopard 2 kutoka Norway hadi ndege za kivita aina ya MiG-29 kutoka Slovakia, Ukraine inaendelea kupokea ahadi za kuipa silaha nzito zaidi kutoka katika mfuko wake mpya wa msaada wa kijeshi wa dola milioni 350.

Lakini vifaru chapa M1 Abrams iliyoahidiwa kupewa hapo awali hakikujumuishwa katika silaha ilizopokea.

Awali maafisa wa Marekani walisema watajaribu kupeleka silaha nchini Ukraine ndani ya muda mfupi ujao.

Mwezi Januari mwanasiasa mmoja nchini humo alisema kutokana na kanuni za usafirishaji, Marekani ina nia ya  kuondoa madini ya Urani katika vifaru hivyo vya Abrams kabla ya kuvituma Ukraine.

Gustav Gressel, mtaalamu anayeshughulika na masuala ya migogoro ya silaha na masuala ya kijeshi katika Baraza la Ulaya upande wa mahusiano ya kigeni ameiambia DW kwamba kile kinachotokea sio kigeni.

Amesema Ukraine itapokea vifaru hivyo ambavyo ni sawa na vile vinavyotumika nchini Misri, Saudi Arabia na Iraq.

Amesema unaweza kuvilinganisha vifaru hivyo na vile vya Leopard 2A4 kutoka Ujerumani ambavyo Norway na baadae Poland zilivituma Ukraine, akisema vifaru hivyo vya zamani badi vina nguvu na ni thabiti kuliko vile vya Urusi.

Lakini ni nini kinachofanya vifaru vya Leopard 2 kuwa chaguo jema katika uwanja wa mapambano?

Kifaru chapa Leopard 2
Kifaru chapa Leopard 2Picha: Christoph Hardt/Panama Pictures/picture alliance

Gressel anasema kanuni za usafirishaji ndio moja ya sababu Marekani inatoa silaha kadhaa kwa Ukraine na nyengine zikiwa zimefanyiwa marekebisho kiasi.

Ameongeza kuwa ndani ya Ukraine kwenyewe kuna masuali mengi yanayoulizwa kwa mfano, kitu gani kitatokea iwapo moja ya vifaru vya kivita vitatwaliwa na Urusi na kufanyiwa uchunguzi.

Wasiwasi huo pia unakwenda mbali kwa makombora ya kujifyatua yenyewe ya M777 ya howitzers ambazo Marekani imekuwa ikizotoa kwa Ukraine tangu mwaka 2022. Aina hizi za makombora zilitolewa bila mfumo wa GPS na Kompyuta za ndani.

Makombora kama haya bila ya vitu hivyo muhimu hukosa shabaha kamili.

Je, Washington inakwepa makabiliano na Urusi 

Rais wa Marekani, Joe Biden
Rais wa Marekani, Joe Biden Picha: Peter Zay/Anadolu Agencypicture alliance

Kulingana na jarida la wall street Marekani ilifanya marekebisho katika makombora yake kabla ya kuyapeleka Ukraine ili kuepuka makombora kurushwa umbali wa masafa marefu hata iwapo Ukraine itapata silaha hizo katika soko la dunia.

Jarida hilo lilimnukuu mtu ambaye hakutaka jina lake litajwe akisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kupunguza hatari ya kutokea kwa mvutano zaidi kati ya Marekani na Urusi.

Mwezi Septemba  msemaji wa wizara ya nje ya Urusi Maria Zakharova alisema kutolewa kwa makombora ya masafa marefu itakuwa ni sawa na kuvuka mstari mwekundu itakayoifanya marekani sehemu ya mgogoro wake na Ukraine.

Stephen Blank, mtaalamu katika taasisi ya utafiti wa sera za kigeni amesema kwa Marekani kudhibiti mifumo yake ya silaha inahusiana na hofu kwa Urusi na kutanuka zaidi kwa mgogoro wa Ukraine na taifa hilo jirani.

Blank amesema lakini haelewi ni kwanini maeneo ya Urusi yanapaswa kulindwa kwa kutoshambuliwa na tayari Urusi imeishaiharibu Ukraine kutokana na mashambulizi yake na isitoshe taifa hilo ndilo lililoanzisha vita.

Amesema vita hivyo ni vigumu na upatikanaji wa ufumbuzi huenda ukachukua muda.