1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Chama cha siasa kali chanyimwa ruzuku ya serikali

Amina Mjahid
23 Januari 2024

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani Die Heimat, zamani NPD, kimepigwa marufuku kupokea ufadhili wowote kutoka kwa serikali kwa miaka sita ijayo.

https://p.dw.com/p/4bbEf
Siasa kali za mrengo wa kulia| NPD
Chama cha Heimat kilitokana na chama cha itikadi kali cha NPD.Picha: Ole Spata/dpa/picture alliance

Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama ya Katiba ya Ujerumani hii leo baada ya mchakato mrefu. Chama hicho cha Die Heimat pia kitaondolewa upendeleo wa kodi inayotolewa kwa vyama na michango ya kisiasa.

Mwaka 2017 mahakama hiyo ya katiba iliamua kuwa chama hicho, wakati huo kikiwa NPD kilikuwa kinayumbisha utaratibu wa kikatiba na kidemokrasia nchini Ujerumani. Lakini mahakama hiyo haikukifungia chama hicho ikisema hakiungwi mkono na wengi na hakitoi kitisho kikubwa.

Soma pia: Korti ya katiba yasema chama cha NPD hakina madhara

Hata hivyo, bunge la Ujerumani lilijibu kauli hiyo kwa kupitisha sheria mpya inayoruhusu vyama vilivyo na siasa kali kutofadhiliwa na serikali na kuondolewa upendeleo wa kodi.