1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkurugenzi wa uchaguzi Tanzania asema anatishiwa

29 Septemba 2020

Mkurugenzi wa uchaguzi katika tume ya uchaguzi nchini Tanzania, Dk. Charles Mahera amewataka Watanzania kutouza vitambulisho vya kupigia kura, akisema hilo ni kosa kisheria.

https://p.dw.com/p/3j9tz
Tansania Wahl Charles Mahera
Picha: Veronica Natalis/DW

Zikiwa zimebaki siku 29 hadi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu nchini Tanzania, mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi nchini hapa Dk. Charles Mahera amesema kuwa pamoja na mafanikio ambayo tume anayoiongoza inajivunia, pia anapitia kipindi kigumu ikiwepo kupata vitisho kutoka ndani na nje ya nchi.

Soma pia: Kampeni zaendelea kupamba moto Tanzania

"Tumeshuhudia watu wa mataifa ya nje, hata mimi hapa nimeandikiwa barua na Mmarekani mmoja anajiita Amsterdam mwanasheria, akiitisha tume ya taifa ya uchaguzi. Kwa sababu watu wanalalamika huko nje kwamba wanaonewa, na kwamba yeye sasa huko nje ndio anajiona ana haki ya kuwajali watanzania kuliko sisi," alisema Dk. Mahera mbele ya waandishi habari katika ukummbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha.

Tansania Wahl Charles Mahera
Viongozi wa kidini, mashirika ya kiraia, mashirika ya walemavu na wadau wengine walioshiriki mkutano na mkurugenzi wa uchaguzi Dk. Charles Mahera, mjini Arusha Septemba, 29, 2020.Picha: Veronica Natalis/DW

"Kwa hiyo mjue kwamba kama taifa ni majaribu tuliyonayo watu muendelee kuyaombea. Unakuta mtu anasimama kwenye jukwaa, anasema fulani atakwenda the Hegue, sasa badala kutumia muda mwingi kueneza sera unaeneza vitisho.”

Soma pia: NEC yashughulikia pingamizi 100 kati ya 500

Maandalizi ya uchaguzi yaelekea kukamilika
 

Mbali na hayo tume ya taifa ya uchaguzi imebainisha kuwa maandalizi kuelekea siku ya kupiga kura oktoba 28 yamekamilika kwa asilimia 80 mpaka sasa huku akitoa onyo kali kwa wale wote wenye lengo la kuuza vitambulisho vyao vya kupigia kura, na kusema kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na wote watakaobainika wanatachukuliwa hatua kali za kisheri.

Akizungumzia suala la kampeni zinazoendelea, mkurugenzi huyo wa tume ya taifa ya uchaguzi amewataka wagombea kuendesha kampeni za kistaarabu na kufuata sheria.

Soma pia:Tume ya uchaguzi Tanzania yamuita Tundu Lissu 

"Kumekuwepo na choko choko na makosa ya makusudi, kusudi mtu fulani afanyiwe fujo halafu alalamike kwamba ameonewa. Tumevumilia sana na IGP amevumilia sana lakini kuanzia sasa mtashangaa, watu watapigwa mabomu wakienda sehemu ambazo wameambiwa wasiende, na tumeona imeanza jana kule Nyamongo Tarime.”

Tansania Wahl Charles Mahera
Baadhi ya wadau wa uchaguzi waliohudhuria mkutano na mkurugenzi wa uchaguzi Dk. Charles Mahera, mjini Arusha, Septemba 29, 2020.Picha: Veronica Natalis/DW

Siku ya Jumatatu, chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kililalamika kurushiwa mabomu ya kutoa machozi na jeshi la polisi, wakati mgombea wa chama hicho alipopita kijiji cha Nyamongo kusalimia wakaazi wa eneo hilo akielekea kwenye kampeni.

Soma pia: Wagombea Tanzania walalamikia uhalifu kwenye kampeni

Walemavu watoa wito wa kuzingatiwa
 

Miongoni mwa wadau walioshiriki kikao hicho ni watu wenye makundi maalumu wakiwepo walemavu, ambao wametoa wito kwa tume kuandaa mazingira yatakayoyawezesha makundi yote wa watu kupiga kura. 

Tume ya uchaguzi Tanzania yawarejesha wagombea 15 walioenguliwa

" Wawekwe wakalimani kipindi hiki cha kampeni ili na sisi walemavu viziwi tuweze kuelewa wagombea wetu wanasema nini ili tuweze kuchagua viongozi bora,” alisema Ramadhani Abubakari, mlemavu wa kusikia ambaye maoni yake yalitafsiriwa na Agness Geofrey.

Soma pia:Tanzania yaihakikishia Marekani uchaguzi utakuwa huru

Tanzania bara na visiwani ina jumla ya majimbo 264 ya uchaguzi, huku idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura wakiwa ni vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 35.

Mwandishi: Veronica Natalis DW, Arusha.