1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Bandika bandua ya makocha ndani ya PSG bado inaendelea

5 Julai 2023

Baada ya kumalizika kwa ligi kuu nchini Ufaransa ya Ligue 1, mabingwa wa ligi hiyo PSG wamemtimua kocha Christophe Galtier aliyehudumu kwa msimu mmoja tu.

https://p.dw.com/p/4TSck
Frankreich Fußball Paris Saint Germain| Pressekonferenz von Trainer Christophe Galtier, Voruntersuchung Diskriminierung
Kocha Christophe Galtier amekinoa kikosi cha PSG kwa msimu mmoja tu na sasa amefungashwa virago.Picha: Fred Dugit/dpa/MAXPPP/picture alliance

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa PSG wamemtimua kocha Christophe Galtier ambaye amekiongoza kikosi hicho kwa msimu mmoja tu.

Bayern Munich kumenyana na PSG Champions League

Licha ya kuipatia klabu hiyo ubingwa wa 11 wa Ligue 1 kwa msimu wake wa kwanza, klabu hiyo tajiri iliweka taarifa rasmi kupitia kurasa zake rasmi za kuachana na kocha Christophe Galtier.

Soma zaidi:Messi azomewa na mashabiki wa PSG uwanjani

Wiki chache baada ya nyota wa PSG Lionel Messikuondoka katika klabu hiyo na kushindwa kwa timu hiyo kutamba katika ligi ya mabingwa barani Uliya kumechangia kwa kiwango kikubwa kwa kocha huyo kufungashwa virago na timu hiyo.

Tetesi zinadai kwamba kocha wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania Luis Enrique kufikia makubaliano ya kukinoa kikosi hicho chenye maskani yake Parc de Princes.