1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya mateka vyaongezeka Algeria

Admin.WagnerD21 Januari 2013

Idadi ya vifo vya mateka wanaoshikiliwa kwenye kiwanda cha gesi cha In Amenas nchini Algeria imeongezeka na kufikia 60 hii ikiwa ni siku ya nne tangu wanamgambo wa Kiislamu wenye itikidi kali wakivamie kiwanda hicho.

https://p.dw.com/p/17O1S
REFILE - CLARIFYING THE NAME AND LOCATION OF THE GAS PLANT Smoke rises above following demining operations at the Tiguentourine Gas Plant, located about 50 km (30 miles) from the town of In Amenas January 20, 2013. Algeria said on Sunday it expected heavy hostage casualties after its troops ended a desert siege, but Western governments warned against criticising tactics used by their vital ally in the struggle with Islamists across the Sahara. REUTERS/Louafi Larbi (ALGERIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS ENERGY)
Algerien Tiguentourine Gasfabrik GeiseldramaPicha: AP

Kuna wasiwasi kuwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka zaidi. Waziri Mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal anatarajia kutoa taarifa zaidi baadaye hii leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu vifo vinavyoendelea kuripotiwa katika kiwanda hicho.

Uvamizi wa kiwanda hicho unaelezwa kuwa ni moja kati ya matukio mabaya zaidi kuwahi kuwakumba wafanyakazi wa kimataifa nchini Algeria ambalo hadi sasa limesababisha kufa na ama kupotea kwa raia wa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Japan, Norway na Romania.

Chanzo kimoja cha usalama nchini humo kinaarifu kuwa jana vikosi vya serikali vilipata miili 25 ya mateka waliouawa na hivyo kuongeza idadi vifo vya mateka kufikia 60 huku idadi kamili ya vifo pamoja na wanamgambo kufikia 80. Katika operesheni hiyo ya jana, wanamgambo sita walikamatwa wakiwa hai na vikosi vya serikali vinaendelea na zoezi la uokozi.

Japan yatangaza vifo tisa vya raia wake

Serikali ya Japan imetangaza kuwa raia wake wapatao tisa wameuawa katika kisa hicho. Japan inasema kuwa imepata taarifa za vifo vya raia hao kutoka kwa serikali ya Algeria hii leo (21.1.2012).

Ujumbe wa serikali ya Japan nchini Algeria
Ujumbe wa serikali ya Japan nchini AlgeriaPicha: Reuters

Vifo hivyo tisa ni idadi kubwa ya raia wa kigeni kutoka taifa moja walioathirika kwa wingi hadi sasa kutokana na kushikiliwa na wanamgambo hao.

Mataifa mbalimbali yameendelea kulaani kitendo hicho cha wanamgambo akiwemo Rais Barack Obama wa Marekani ambaye raia wake mmoja amethibitika kuuawa katika tukio hilo.

Ujerumani yatoa rambirambi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema kuwa nchi yake inalaani mauwaji hayo na kwamba wako pamoja na familia za wafiwa katika wakati huu mgumu wa maombolezo na wasiwasi.

"Tunaungana na familia za waathirika katika wakati huu wa majonzi, familia za Waalgeria, pamoja na familia za wageni", alisema Wetserwelle.

Guido Westerwelle, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani
Guido Westerwelle, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Pamoja na Westerwelle, naye Waziri Mkuu wa Uigereza David Cameron amesema tukio hilo ni alama ya kuikumbusha dunia juu ya hatari kuwa ya magaidi. Raia sita wa nchi yake wanashukiwa kuuawa katika mkasa huo. Raia wa Algeria pia wameuawa katika mashabulizi hayo.

Mfanyakazi mmoja katika kiwanda hico raia wa Algeria aliyejitambulisha kwa jina la Abdelkader ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa wanamgambo hao walikuwa wanajua ramani yote ya kiwanda hicho na walikuwa na taarifa za kutosha.

Vikosi vya Algeria katika harakati za kuwaokoa mateka
Vikosi vya Algeria katika harakati za kuwaokoa matekaPicha: picture alliance/abaca

Anasema walipovamiwa walianyang'anywa simu zao na kisha kamera za ulinzi zilivunjwa kabla ya watu kuanza kuuawa. Wanamgambo hao waliwaambia kuwa watu raia wa Algeria wasiwe na wasiwasi kwani wao wanawataka wageni ambao mataifa yao yanawauwa ndugu zao huko Mali pamoja na Afghanistan.

Miili ya watu waliokufa inaarifa kuharibiwa vibaya na manusura wanasema kuwa walishuhudia wenzao wakilengwa kwa risasi vichwani, kurutwa na kufanyiwa unyama wa hali ya juu.

Mwandishi: Stumai George/Reuters/Afp

Mhariri: Mohammed Khelef