Deutsche Welle: Hali yazidi kuwa ya wasi wasi nchini Senegal kabla ya uchaguzi wa Rais Jumapili ijayo.
Ligi Kuu ya Kandanda hapa Ujerumani - Bundesliga inaelekea ukingoni. Baada ya bingwa kujulikana sasa macho yote yamegeuka katika nafasi za kucheza kandanda la Ulaya. Kwa mengi zaidi kuhusu mechi za wikiendi hii Suleman Mwiru amezungumza na Bruce Amani kuhusu michezo ya wikiendi hii na ambao utatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa DW Kiswahili na kupitia redio mbalimbali washirika.
Katika kijiji cha Mbyo nchini Rwanda, Watutsi ambao walinusurika katika mauaji ya halaiki na madhira mengine sasa wanaishi pamoja na wahalifu wa Kihutu waliorekebishwa tabia. Lakini wameiambia DW kuwa haikuwa rahisi.
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.