1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Tanzania yakiri kumshikilia kada wa chadema

Admin.WagnerD4 Julai 2022

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, limekiri kumshikilia Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana la Chadema(BAVICHA) Twaha Mwaipaya, akituhumiwa kwa makosa ya kimtandao.

https://p.dw.com/p/4DeDj
 Inspector General Polizei  Tanzania IGP Simon Sirro
Picha: Police Communications Department

Kufuatia hatua hiyo chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema wameelani tukio hilo na kulitaka Jeshi hilo, kufuata misingi ya sheria badala ya kuvunja haki za binadamu kwa viongozi wa chama hicho.

 Akielezea tukio la kukamatwa kwa Mwaipaya, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Masuala ya Mambo ya Nje, wa Chadema, John Mrema alisema Twaha alikamatwa wakati akiwa njianio kurejea Dar es salaam akitokea Dodoma kwenye shughuli za chama.

"Walimwambia anashutumiwa kwa makosa ya mtandaoni" Mrema aliiambia Dw na kuongeza kwamba kiongozi huyo wa vijana alikamatwa mjini Mrogoro na kupelekwa kituo cha polisi cha kati.

Soma pia:Kiongozi wa upinzani Tanzania aachiwa huru

Aidha chama hicho kilipata taarifa kuwa mwanasiasa huyo alisafirishwa leo alfajiri hadi mjini Dodoma ambako anatuhumiwa na kufikishwa katika kituo cha polisi kikuu.

Mfululizo wa kukamatwa kwa viongozi wa chama hicho

Kwa kipindi cha miaka mitano viongozi wa chama hicho kikuu cha upinzani ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wake Freeman Mbowe pamoja na wananchama wengine wamekuwa wakijikuta kwenye vyombo vya sheria kutokana na tuhuma mbalimbali.

Chama hicho, katika kile walichokiita kusaka haki ya kada wake, kimewataka mawakili kufungua mashauri mawili ya msingi mahakamani.

Tansania Dar es Salaam Freeman Mbowe Oppositionspartei Chadema
Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe Picha: Eric Boniface/DW

Shauri la kwanza lifunguliwe katika mahakama ya hakimu mkaazi Kisutu jijini Dar es salaam kulitaka jeshi la polisi limpe dhamana kiongozi huyo wa vijana.

shauri la pili lifunguliwe katika mahakama kuu Dodoma kulitaka jeshi la Polisi limfikishe mahakamani au limpe dhamana kiongozi huyo ambae mara kadhaa ameonekana kutumia mitandao ya kijamii katika kusukuma mbele ajenda za kisiasa na kimtazamo.

tayari mawakili wa chama wamefungua wamefungua kesi mahakamani jijini Dodoma kuwalazimisha Polisi kumwachia kwa dhamana mwanachama wao Twaha Mwaipaya.

Soma pia:Rais Samia: Tanzania haiwezi kujengwa na chama kimoja

Wakili Fredrick Kalonga amesema tayari wameshapeleka maombi hayo leo Jumatatu 4 Julai 2022 mahakamani na hadi leo mchana walikuwa wanasubiri kupangiwa Jaji na kupewa namba ya kesi.

Kwenye maombi yao Chadema, mbali na kuwashitaki Polisi, wamemshitaki pia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kwenye maombi yao kikubwa wanaomba Mwaipaya aachiwe kwa dhamana au kesi ipelekwe mahakamani haraka.

 Polisi yakiri kumshikilia mwanasiasa huyo

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amekiri kushikiliwa kwa kiongozi huyo wa baraza la vijana wa chama kikuu cha upinzani.

Alisema bado wanamshikilia mwanansiasa huyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi  kutokana na mashtaka anayotuhumiwa nayo.

 Kushikiliwa kwa Mwaipaya katika kituo cha polisi Morogogo kwa siku kwa siku kadhaa kulizua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii, wakishinikiza jeshi la polisi kumuachia mwanasiasa huyo kijana.

Mbowe na wenzake watatu waachiwa huru