Ghasia zimeendelea nchini Ugiriki baada ya mamia ya vijana wanaopinga mipango ya serikali ya kubana matumizi kupambana na polisi.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa lilipitisha kwa wingi mkubwa wa kura azimio linalounga mkono Palestina kuwa mwanachama kamili wa umoja huo.
Ujerumani imelaani ongezeko la ghasia dhidi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huko Jerusalem Mashariki.
Kiongozi wa Chama Kikuu cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Keir Starmer amesema hii leo wataufutilia mbali mpango wa serikali ya Conservative wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ikiwa wataingia madarakani.